Friday, December 27

Mapishi ya Salad

Karibu katika mapishi ya salad ambapo wale wanaopenda kujiweka fiti watanielewa naongelea nini.

Mahitaji:

  • Kamba - kilo 1
  • Karoti - kilo 1
  • Broccoli - kilo 1
  • Maharagwe machanga - kilo 1
Hatua:
  • Osha kamba wako vyema ukihakikisha wametoka mchanga wote
  • Katakata karoti, broccoli na maharagwe machaga katika ukubwa uupendao 
  • Chemsha kamba peke yake, ukiweka chumvi kiasi pamoja na pilipili manga iliyosagwa kidogo. Chemsha kwa muda wa dakika 20 - 30 huku ukionja kama wameiva vyema
  • Chemsha karoti pamoja na broccoli huku ukiongeza chumvi kiasi kwa ajili ya ladha 
  • Chemsha maharagwe machanga peke yake kwani yanatumia muda zaidi kuiva kuliko vya juu.
  • Changanya vyote baada ya kuiva vyema, koroga ukihakikisha vimechanganyika vyema
  • Ongeza salad dressing uipendayo na chumvi kiasi kama wapenda
  • Salad yako ipo tayari kwa kuliwa


Dressing  salad ambazo sisi tulizitumia katika salad yetu

  Tunakutakia wikiendi njema na yenye baraka tele, huku ukiendelea kututembelea kuona yalojiri humu jikoni kwetu.

No comments:

Post a Comment