Thursday, November 7

Wali wa nazi toka kuleeeee Lindi

Kama tulivyoshasema hapo awali kuwa watu wa Lindi ni wazuri sana katika upishi. Sasa basi kwenye upishi wa wali shurti tui la nazi linahusika, na kuwa kujua hilo, tukaagiza menu kama itakavyojieleza hapo cihini kwa picha.
   Kuna wali wa nazi, maharagwe ya nazi, pamoja na samaki wa mchuzi wa nazi, ndo moja ya menu tulipata kula tukiwa Lindi.

   Rafiqs ili nawe uweze pata menu kama hiyo yenye tui la nazi, basi tumia tui la pili wakati unachemsha maji wa wali, na pia waweza tumia tui la kwanza iwapo utapenda utamu ukolee vyema.
   Baada ya kupika share nasi picha ya wali wa nazi, na utujuze utamu wake.

No comments:

Post a Comment