Friday, November 8

Tumerejea Dar iliyo Salama

  Dar iliyo salama ndio jiji tunaloishi, koteeee tunatembea kisha twarejea nyumbani,,,,, walishasema nyumbani ni nyumbani. Ile kufika tu, tukakuta dada ameandaa ndizi nyama moja matata sana, ghafla tukahisi tupo Rombo mkuu kwa bibi.
  Kwa picha ndio ndizi nyama yenyewe katika sahani yangu....
 
Kusindikizia mlo huo, kuna kachachandu kalitengenezwa kwa pilipili na maembe kisha ikapikwa flani hivi..... utamu mtupu.
    
kutoka Dar iliyo salama, twawatakia Wikiendi njema yenye mapumziko safi.

No comments:

Post a Comment