Monday, November 11

Menu ya kitaani - Samaki

   Baada ya wiki nzima ya kuwepo Lindi, tumerejea Dar iliyo Salama, na tumeendelea na misosi ya hapa na pale.
   Menu ya leo tulipishana nayo canteen za ofisi za Airtel siku chache zilizopita. Yale mambo ya menu mboga saba. Kuna wali mweupe, Samaki mchuzi, mboga za majani pamoja na maharagwe, huku vyote vikisindikizwa na kachumbari.

    Jaribu kukisia menu hii inagharimu kiasi cha shilingi ngapi za kitanzania, na iwapo utakuwa wa kwanza kujibu kwa jibu sahihi, basi zawadi tamu yakusubiria kwa hamu.
   Tutumie jibu lako kupitia anwani hii ya barua pepe, menutimes@gmail.com
 Menu time tunawatakia wiki njema yenye mafanikio.

No comments:

Post a Comment