Tuesday, November 12

Zijue faida za samaki mwilini

 Kutoka kwa samaki, mwanadamu anafaidi mengi ukiondoa utamu. Humu hupata viruubisho kama vitamini D na B2, ndio madini ya chuma, zinc, iodine, magnesium, na potassium hupatikana.
Faida za samaki mwilini  ni nyingi zikiwemo hizi hapa chini:-
•Huyeyusha damu ma kuifanya iwe nyepesi  
• Huilinda mishipa ya damu isiharibike
• Huzuia damu kuganda
• Hushusha shinikizo la damu

• Hupunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo na kiharusi

• Hutuoa ahueni kwa wenye ugonjwa wa kipandauso

• Husaidia kuzuia uvumbe mwilini

• Huendesha mfumo wa kinga ya mwili

• Huzuia saratani

• Hutoa ahueni kwa wenye pumu

• Hupambana na dalili za awali za ugonjwa wa figo

• Huongeza nishati ya ubongo

    Zipo sehemu nyingi ambapo samaki hupikwa na kuuzwa, yaani migahawani, mahotelini n.k, pia sehemu mbalimbali zinazouza samaki katika bei tofauttofauti na mtindo tofauti, mfano magengeni, feri, sokoni ambapo utapata samaki wabwachi au walioshapikwa. 
Baada ya kusoma na kuelewa umuhimu wa samaki ndani ya miiili yetu, tujitahidi mara kwa mara kupata mlo wa samaki
   Samaki huyu tulikutana naye kule Coco beach iliyopo Dar iliyo salama.
    Yaliyomo kwenye sahani ni ugali mweupeeeee, mboga za majani, maharagwe na ile mboga kuu ambapo ni samaki wa mchuzi aloungwa kwa tui la nazi.
    Hapa samaki huyu amekaangwa kwanza kabla ya kuungwa mchuzo na kuongezewa nakshi ya tui la nazi. Tutaja kuwafunda pishi hili siku za usoni, pamoja na mapishi mengine tuliyoyaahidi.
   Rafiq, upatwapo na hamu ya kula samaki na kuongeza virutubisho byake mwilini, je ni sehemu gani hupenda kuwatembekea na kukidhi hamu yako?? Au iwapo wamnunua mbichi, ni soko lipi huwa unakwe kuwanunua?? Tujuze nasi tuweze kuwatembelea.

No comments:

Post a Comment