Wednesday, November 13

Samaki wa Kawe

Baada ya kujua na kufahamishana kuhusiana na faida za samaki, tumeona tuendelee kuwatafuta wapatikanapo.
   Moja ya sehemu ambapo wanadarisalama wengi hupendelea kwenda kupata samaki ni Kawe beach. Huko utakutana na samaki safi kabisa, wapo wengi tayari kwa kuliwa na wewe.
   Tulipofika baada ya dakika kadhaa, mezani tuliletewa menu hii hapo chini. Samaki choma pamoja na ndizi za kukaanga, huku tukisindikizwa na kachumbari
   Karibu kutujuza sehemu zingine watengenezapo samaki tupate kuwajulia hali na kuwatangaza. anwani yetu ni www.menutime.blogspot.com
   Tunawatakia Jumatano njema yenye mafanikio.

No comments:

Post a Comment