Thursday, November 14

Kitaa kipya cha menu pande za Mikocheni

   Ukiwa unatokea mitaa ya Rg yaani Rose garden kama unaenda kwa Mwl Nyerere kwenye kona baad ya maghorofa ya TPDC, kuna kaoutlet kapya hivi, kamenakshiwa na viti vyenye vitambaa vya kijani.
Ukiangalia huachi kupaona, pako very visible. Tulifika pale kupata cha mchana katika kubadilisha mandhari ya sehemu za kupata mlo.
  Mmoja wetu alipata menu hiyo hapo chini, wali wenye njegere kwa mbali, maharagwe ya nazi, mchuzi na kuku mkavu, huku kwa pembeni mboga za majani zikimsindikiza taratiiiibu kuuona mchana wake
   Kuna sehemu nyingi zimefunguliwa zitoazo huduma ya vyakula katika mida tofauti tofauti. Karibu kutujuza wapi pamefunguliwa papya tupatembelee, tupatathmini na kama panafaa tupapaishe kama tufanyavyo.

No comments:

Post a Comment