Wednesday, November 6

Cha mchana kutoka Lindi

  Siku tunaingia Lindi kutoka Mtwara maana tuliendesha ilikua ni mida ya mchana hivi, na kwasababu tulikua na njaa tuliwaomba wenyeji wetu watuonesha wapi tunapunguza kelele za tumbo, na tulipelekwa Himo restaurant, ambapo tulifahamishwa ni maarufu sana.
   Fasta tuliagiza kuku wa kienyeji pamoja na viepe, hapo chini ni muonekano wake

  Chipsi zilinoga maana zilikua ndo kwanza zimetoka jikoni, safiiiiii na tamu. Pembeni kisindikizio chachandu kilihusika

   Zaidi ya mengi ambayo tumeshaonesha, kuna mengine yanakuja na tunandelea kukujuza kutoka Lindi. 
usisahau kupita hapo Himo, wana juisi ya ukwaju, chai ya rangi na tangawizi na mengine mengi matamu.
   Tunarejea Alhamisi, yaani kesho.

No comments:

Post a Comment