Tuesday, November 5

Supu ya Kyoo wa Kienyeji toka Lindi

  Siku zinazidi kusonga mbele wakati huo bado nasi tuliokuwepo Lindi, katika pitapita yetu, kama wapenda misosi tukapishana na supu ya kuku a.k.a kyoo wa kienyeji.
  Kwa kweli tulipokua tunamla, tulidhani ni wa kisasa, maana alikua mlaini mno. Pata picha ya muonekano wake

    wakati twafaidi ya lindi, dada yangu Bi Hamida......huwa napenda kumtania sana, alishare nami supu alikua anapata mida hiyo hiyo huko Dar es Salaam, katika baa ya Shieni iliyopo Sinza. Pata muonekano wa supu yake
   Kama wewe pia ni mpenda supu, karibu kushare nasi picha ya supu na tujuze wapi umeipata. Ila kesho tutarejea tena kuendelea kuwajuza menu toka Lindi.
   Siku njema kwenu Rafiqs!!

No comments:

Post a Comment