Monday, November 4

Kifungua Kinywa toka Lindi

   Mwisho wa wiki iliyopita tulikuwa mkoa wa Lindi, na kwasababu tulilala na kuamkia Lindi, tukaona ni vyema tukiwajuza tulifungua vinywa vyetu na menu gani.
   Mkoa wa Lindi ni mafundi katika upishi atiiii, sasa asubuhi tulikutana na menu ifuatayo :
Sahani yangu ilisheheni mkate wa kumimina, kitumbua pamoja na kalimati, huku nikivisindikiza vyote na chai ya maziwa iliyopikwa na viungo

  Patna yeye sahani yake asubuhi ile ilisheneni andazi lenye iliki pamoja na kitumbua akishushia na chai iliyopikwa kwa viungo kama mimi.

   Kwa wiki nzima tutakuwa tukiwajuza menu tulizozipata huko Lindi katika safari yetu, ili ujue iwapo utatembelea Lindi ni menu zipi utapishana nazo.
   Kutoka Lindi, Ljm wa Menu Time nawahabarisha!!

No comments:

Post a Comment