Wednesday, October 30

Pizza pizza pizza !!

   Pizza ni moja ya vyakula ambavyo twapenda sana, lakini inategemea inapatikana wapi. Saverio's ni moja ya sehemu ambayo mara zote huwa napenda kwenda kupata pizza. Moja ya kinachonivutia ni sauce ya vitunguu swaumu ambayo inawekwa na viungo vingine.
  Chini ni moja ya pizza tuliyowahi kuipata siku za karibuni.

   Kutoka pande za Mikocheni, naongelea Shoppers Plaza, kuna  eneo pale paitwa Flirtease, na hapo tulikutana na chicken pizza, kama ionekanavyo hapo chini.

  Tujuze ni menu gani waipenda sana na huwa waipata maeneo gani, ili tuweze kushare na Rafiqs wengine.

No comments:

Post a Comment