Kama ilivyo ada ifikapo siku za Ijumaa yaani tuanzapo wikiendi, tujulishane je, mtoko wa wikiendi ni wapi, na wapi tupate menu ya maana.
Leo tupo Qbar, tunaangalia misosi iliyopo. Pale utapata mlo, vinywaji vyenye ulevi na visivyo na ulevi, huku ukiburudishwa vyema na muziki mzuri toka Borabora band.
Tuangalie baadhi ya menu zinazopatikana pale.
Kuku waliopikwa wakapikika vyema, na utamu ukawa mahali pake wanapatikana pale katika malipo ya kawaida sana.
Halafu kulikua na viepe vilivyosindikizwa na kitimoto kilichookwa na viungo vya aina yake.
Kwa wale wenzangu na mie wapenda vya majini, kamba a.k.a prawns wanapatikana katika mapishi tofautitofauti.
Wapo kule Oysterbay kwenye kona kabla ya jengo jipya, baada ya supermarket ya Shrijees. Ukifika mtafute Moody, au sema na mhudumu yeyote upate kitu roho inataka.
Twawatakia wikiendi njema ninyi na familia na Rafiqs zenu.
No comments:
Post a Comment