Friday, October 11

Home made supuuuu ya Ng'ombe

   Iwapo una mume ambaye hupenda kwenda kunywa na marafiq siku za Ijumaa, wala usipate presha ati kesho yake akatafute supu sehemu za baa.
  Ukiwa nyumbani kwako waweza mpikia supu mumeo na pale akiamka wampatia na kusaidia kukata mning'inio kisha akashushia na maji bariiidi tayari kwa siku mpya.
   Mimi niliweza pika supu hii hapa, na ntarejea kuwajuza namna gani ya kuipika ikapikika na utamu ukawa sawa kama si zaidi ya zile wapikazo kuleeee.... si wapajua!!
Karibu kushuhudia

   Rafiqs hakikisha una ndimu, pilipili na chumvi kama viongeza vikorombwezo ndani kwako, maana vina ladha yake katika unywaji wa supu.
   Ijumaa ndio hii,Rafiqs jipange mumeo akirejea umpikie kesho yake, na sio lazma awe na mnin'ginio, la hasha, hii ni mchemsho ambao ni menu nzuri haswa kwa wale wasiopenda vyakula vya mafuta.
Wikiend i njema twawatakia

No comments:

Post a Comment