Monday, September 23

Tambi na nyama ya ng'ombe

   Baadhi ya wana Menu Time wapo pande za Kahama, pachimbwapo  madini..... wamekuja salimia partners wengine wa Menu Time. 
  Na kama ilivyo ada popote pale walipo wana Menu Time, shurti ufundi uoneshwena menu itengenezwe. Na leo chakula cha mchana tumepika macaroni na nyama ya ng'ombe yenye sosi ya jibini na maziwa.
  Namna ya kupika menu hii angalia mapishi ya macaroni

  Katika picha ya ukaribu zaidi, tuliongezea njegere kidogo
    Hakika menu ilikua tamu muno...... wenyeji wetu walifurahia na pia wameshukuru. Tujuze mchana huu umepata menu gani na wapi??

No comments:

Post a Comment