Thursday, September 12

Nyama choma Festival iliyobamba siku ya Jumamosi

   Moja ya ujuzi wetu au tuseme mapishi tunayojivunia timu ya Menu time ni utengenezaji wa salad ambapo tulifundishwa vyema na mama yetu.
   Katika tamasha la Nyama Choma lililofanyika siku ya Jumamosi tulihudhuria na pia kushiriki katika uuzaji  wa salad tukishirikiana na partners wetu tuliowatambulisha rasmi wana Legitimate.
 Leo tutaongelea Salad iliyokuwepo, kulikua na ile kachumbari ya kiswazi, yaani ile ya kulia pilau, nyama choma, ugali samaki 
  Hapa wapata picha ya salad zote mbili

Kwa ukaribu kabisa, pata kuona salad ya uswazi kama tuiitavyo yaani kachumbari, full kukolea ndimu.

Halafu kuna ile ya kishua yenye mayonnaise, ambapo tumeweka mambo matamu na siri ya mpishi humohumo.

  Tuwashukuru wale wote walituunga mkono siku ile ya Nyama choma kwa kununua salad zetu, kwa kututembelea kutujulia hali na pia kwa kututangaza.
   Kesho twarejea kuwajuza nyama ilikuajeeee.....
Jitayarishe jumamosi hii tunachoma nyama tena pande za Leaders.

No comments:

Post a Comment