Friday, September 13

Nyama choma festival

   Tunamalizia kuhabarisha matukio ya Jumamosi iliyopita ambapo tunamalizia na nyama zilizokuwepo zinachomwa na Legitimate.
   Hatuongei sana.... karibu uone... palikuwepo na kuku na mbuzi pia
 

Mbuzi kwa ukaribu kabisa, chaguo lilikua lako kama uwe mguu au mbavu, chochote upendacho, sisi tulikua radhi kukuuzia

 Tukashauriana, kwanini tusitafute T-bones tuzitengeneze vile zinatakikana na kisha tuuze???

 Wachagga wachagga tu, kwenye nyama shurti ndizi choma iwepo maana yahusika sana kwenye hili zoezi


 T-bones zikiwa tayari kwa kuliwa, kwa picha ya karibu kabisa, ambapo kwa kuiangalia waweza kadiria utamu wake. 

   Asanteni sana kwa support yenu Rafiqs, kwa kuwa wateja wetu na kwa kuturuhusu kuwahudumia. Tunaamini mlifurahia huduma zetu Menu Time pamoja na Legitimate. 
Iwapo tulikosea twaomba radhi kwa hilo.
   Tunajipanga na Jumamosi hii... habari itakua ni Leaders ground, ambapo kuna Kilimanjaro Music Tour Kikwetu kwetu zaidi, tukiwasindikiza wasanii kibao wakiwemo Lady Jaydee, R.O.M.A na wengineo.
Karibu sana rafiqs, tutakuwepo twawapikia nyama, chipsi na mengine mengi... Team Menu Time!! 

No comments:

Post a Comment