Siku ilikua nzuri sana, jua kidogo na upepo kwa mbali, marafiqs mbalimbali wakienjoy na kupeana kampani, huku wengine wakituunga mkono pale Menu Time tulikuwepo.
Tusiseme sana.... yalojiri..... tuangalie sote kwa picha zifuatazo,
Muonekano wetu ulikuwa hivi....
Matayarisho yalianzia hapa.... vitunguu vilimenywa tayari kwa pilipili pamoja na kachumbari
Nyama ilitayarishwa tayari kwa kutungwa kwenye vichomeo nyama a.k.a skyuuz
Baada ya kuwekwa viungo kadha wa kadha, ikatungwa tayari kwa kuwekwa juu ya jiko na kuchomwa
Tulihakikisha wapo wa kutosha na pia walipikwa kwa style tofauti, kwani kuna waliochomwa na kuna waliokaangwa.
Moja ya kiungo muhimu katika mapishi, haswa nyama choma ni pilipili, hapo ikiwa inaivishwa
Wapenzi wa sausage hatukuwasahau, tuliwapa kile roho yao inapenda.
Nyama choma, besti yake ni pilipili, mambo yetu yale na ndizi, hivyo tuulihakikisha uwepo wa ndizi, tena zile mzuzu ambapo zilipatikana zile tamu na zile mbichi
Pale panapohusika, sehemu ya kujidai na kujinadi, yaani wanja wa mchezo ndo ulikuwa hivi
Timu Menu Time wakiwa kazini... twapenda kusema kazi kazi .... Vijana wapo kazini
Kesho tutawaonesha, baada ya kuiva mambo yalionekanaje.... tupende a.k.a like us kwa face book page yetu www.facebook.com/MenuTime uzidi kuhabarishwa zaidi.
Jumatatu njema na wiki njema yenye mafanikio.
No comments:
Post a Comment