Tuendelee kuona baada ya kuwiva, menu ilionekanaje?
Dada yangu hupenda kuwaita hawa vyuku ati wako wengi
Wapo tayari kabisa kwa kupakuliwa na kuliwa.
Mishkaki ikiwa jikoni ikichomwa kwa umahiri mkuu
Viazi a.k.a viepe a.k.a chipsi zikiwa zinaepuliwa tayari kwa kuuzwa kwa mteja
Miguu ya kuku ilikuwepo, waswahili ati wanasema ukiila sana hii, unakua na safari nyingi nyingi katika maisha yako, yaani hutulii. Sasa msemo wao unakuwa "anatembea/ anasafari huyu kama kala miguu ya kuku..." Waliopata kuila walizunguka eneo lile vya kutoshaa
Muonekano wetu ulikuwa hivyo tukikujulisha toka kwa mbali uwepo wetu.
Kihalali ilikua ni siku nzuri kabisa kwa wale tukiohudhuria, kimauzo, kistarehe, kikazi, kirafiki n.k.
Tuwashukuru sana partners wetu wana Tongwe records, cousin wetu bwana Danny Lema, marafiqs waliohudhuria siku hiyo, wasanii waliotuburudusha na waandaaji wa shughuli nzima TBL kupitia bia yao ya Kilimanjaro yenye Bonge la kiburudisho, EARadio, Front line, Integrated Communication na uongozi wa Leaders.
Kutoka viwanja vya leaders, LJM wa Menu Time naarifu
No comments:
Post a Comment