Nelwa Gelato walikuwepo pande za Botanical garden wakionesha ufundi wao wa utengenezaji wa ice cream.
Hebu angalia ladha kadha wa kadha ambazo wanatengeneza
Kuna ladha za strawberry, vanilla, chocolate na nyinginezo nyingi, ambapo tulipozijaribu kwa kweli utamu wake hauelezeki. Wapo sehemu kadhaa wakiuza bidhaa zao za ice cream
Kutoka Arusha, tulikutana na Rafiqs ambao wao wana bidhaa tofauti tofauti, yaani wanatengeneza asali, kahawa na pia wanafanya ukarabati wa mashine za kutengenezea kahawa.
Cha kwanza tunaangalia ni asali wanazotengeneza wenyewe na kuziuza kwa jumla ya fedha taslimu za kitanzania shilingi elfu kumi tu.
Kahawa zao hupakiwa katika mtindo huu, hivyo ukiona packaging hii jua una bidhaa ya ukwe'ee
Wanaitwa EDELWEISS Coffee Estate, Arusha wanapatikana Njiro
AK's cafe nao hawakubaki nyuma, walionesha msosi wa kwanza ni pasta yaani tambi
Pia walikua na veggie rolls ambazo sauce waliyotumia hakika iliongeza utamu wa pekee, kwa namna ya kipekee
Walionesha ujuzi wao kwenye upande wa vimiminika pia
Na burger zao walionesha nembo ya eneo lao la kazi, kwa kuweka vipeperushi vyenye jina lao
Upande wa mwisho walikuwepo Rafiqs ambao hatutawaongelea sana angalia mwenyewe sanaa ya urembo na mapambo
Yummyy
Pembeni kulikuwa na viunganishi hivi.....
Hakika kila mpishi ana namna yake ya kuonesha kivutio cha menu yake kwa walaji wake
Kihalali tulienjoy sana kuwepo pale na kuweza kuchukua machache ambayo tumeweza waonesha hapa. Tunaamini mmepata vyema kujua yalojiri.
Kesho tutaona yaliyojiri kwenye Nyama choma festival ambayo tulihudhuria na kushiriki baada ya kutoka hapa.
No comments:
Post a Comment