Tuesday, September 10

Dar es salaam Food Fair Event yaendelea kuhabarishwa

 Tunaendelea kukujuza yalojiri siku ile ya Jumamosi pande za Dar es salaam National Botanical Gardens mitaa ya Garden Avenue.
  National Collegue of Tourism waliopo Ohio street nao walikuwepo wakiwa wanaonesha utaalamu wa mapishi yao.
  Kulikua na mishkaki ya nyama

  Mishkaki ya matunda

   Na pia kulikua na mishkaki ya mbogamboga ambayo ilikua mitamu sana

  Rafiqs wengine walikuwepo na mambo mengi mengi matamu. Kulikua na kashata kubwa kubwa

 Kulikuwa na keki ndogo ambazo zilikua na utamu wa pekee
   Ukiondoa keki, walituonjesha cookies pia, ambapo kulikuwa na zenye mbogamboga, matunda na za nyama
  

Kwa wale wenye meno matamu a.k.a sweet thooth

   Ukipiga simu namba 0687 043 502 utawapata, wao wapo nyumbani, utaongea nao na watakupatia cookies na candy mbalimbali, angalia mojawapo za bidhaa zao


    
   Kuna hivi visweet ambavyo vina ladha ya ajabu yaani mwishoni ndio inalipuka kiana mdomoni. Watafute uonje bidhaa zao
 
    Kesho tutamalizia vyote vilivyotokea siku ya Jumamosi, pale wapishi wa aina mbalimbali walipokutana mitaa ya dar es salaam, Botanical garden.

No comments:

Post a Comment