Monday, September 9

Dar es salaam Food Fair event - Habari

   Jumamosi iliyopita ya tarehe 7 ya mwezi huu wa tisa, kulikuwa na tukio lililoitwa Dar es salaam Food Fair ambapo ilifanyika eneo lijulikanalo kama National Botanic Gardens, Garden Avenue.
   Wengi wahusikao na mambo ya maakuli walikuwepo, kutoka mikoa mbalimbali hapa Tanzania.
   Epid'or Cafe, Bakery & Restaurant walikuwepo, na  walivyovionesha ni hivi hapa chini...




   Malaika Caffe waliopo kona ya The Slipway na Chole road nao walikuwepo, wakionesha ujuzi wao katika utengenezaji wa vinywaji moto mbalimbali vikiwemo capuccinno na vinginevyo.
  Muonekano wao ulikuwa hivi...


   Njombe Milk Factory kutoka mkoa wa NJombe nao walikuwepo wakionesha ujuzi wa utengenezaji wa jibini a.k.a  cheese


   Mchanganyiko wa jibini na matunda yaani nyanya na black olives ulikuwepo

  Jibini zilizowekwa pilipili manga zilikuwepo


Jibini zenye pilipili zilikuwepo


   Kwa picha ya pamoja ya jibini muonekano ulikua hiviii


   Chocolate Mamas ambaye ni watengenezaji wa chokolate  walikuwepo pia. Walisema wao wanakuletea kwako, au unachukua kutoka walipo. Namba zao ni 0789 380 807


Walitujuza kuwa chokoleti inakwenda vyema sana na bilauri ya mvinyo

   Nembo yao ni hii hapa
 
  Tutarejea kuwajuza zaidi yaliyojiri hapo kesho

No comments:

Post a Comment