Tuesday, September 3

Home made Kifungua kinywa

Leo tulijipikisha asubuhi fasta fasta kabla ya kuingia mzigoni na kama kawaida yetu mapenzi yetu yapo kwenye mayai ya kuvurugwa ambapo yana mchanganyiko wa viungo vifuatavyo... chumvi, asali, maziwa, jibini, nyanya na kukaangwa na blue band badala ya mafuta ya kupikia.
   Pembeni mayai hayo yalisindikizwa na chapati, andazi na sambusa na kushushiwa na chai ya maziwa.

  Namna ya kupika mayai hayo ni weka kikaango motoni, ongeza blueband na chumvi, kisha weka vipande vya nyanya, acha vikaangike kisha ongeza maziwa na asali kidogo, koroga mpaka rojo lijitengeneze. 
  Ongeza mayai uliyoyakoroga pembeni, koroga kiasi kisha malizia kuweka jibini, yakoroge kwa mtindo wa kuvuruga mpaka yakiwa yameiva kabisa, kisha epua tayari kwa kuliwa.
   Kesho tujuze wafungua kinywa vipi????

No comments:

Post a Comment