Wednesday, September 4

Fungua kinywa na Chai ya rangi

   Kuna baadhi ya rafiqs ambao hawawezi kabisa kunywa chai asubuhi, na wengine hawawezi kunywa chai ya maziwa, yaani maziwa yaliyochemshwa na kuongezwa majani ya chai, au kahawa n.k. 
  Kuna wale wapendao chai ile ya kuchemsha maji kisha kuongeza aidha majani ya chai, au kahawa, au viungo vinginevyo kama tangawizi n.k.
   Rafiq ameshare nasi chai ambayo huinywa mara kwa mara ambayo ni ya rangi yaani maji yalochemshwa na majani ya chai na kuongezwa sukari, ambapo alisindikizia na chapati pamoja na maandazi.

  Asante kwa kushare nasi mlo wako wa asubuhi, japo hukutupatia jina lako.
 Rafiqs, tembelea page yetu kwenye face book ukifuata www.facebook.com/MenuTime ambapo utajuzwa mengi yatokeayo hapo kwa hapo. Na pia jumuika nasi siku ya Jumamosi ijayo tarehe 7, tutakuwepo Posta ground kwenye Nyama choma festival tukiwatambulisha vijana wa Legitimate.
  Rafiqs, endelea kututembelea kujua zaidi shughuli zijazo kuhusiana na Menu Time.

No comments:

Post a Comment