Chakula ni kiungo muhimu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu, katika hali ya kawaida huwezi kupitisha siku bila kuwaza kuhusu nini utakula,
Hapo kuna wali mchafu yaani pilau, kachumbari, nyama ya kuku na ng'ombe pamoja na ndizi
Chakula kinaweza kutumika kama suluhisho kati ya watu ambao hawana maelewano mema, mfano kama kuna watu wamekwazana na unapenda kuona wanapatana na kurudi kuwa marafiki basi tumia chakula kuwaunganisha. Unaweza ukapika chakula kwako na kuwakaribisha wote wawili waje kula chakula pamoja ama waweza kwenda hotelini na mkashiriki nao mlo pamoja.
Na mwaweza anza na matunda
Na mwaweza anza na matunda
Ukiondoa kukutana nyumbani mwaweza toka mkaenda mgahawani na kuyamaliza
Chakula bado ni kiungo muhimu pia katika shughuli mbalimbali, Sherehe za Harusi, Kitchen Party, Sikukuu za kuzaliwa(Birthday).
Muonekano wa wapi menu inawekwa ni muhimu sana ili kuwapa hamu ya kula wale walaji wako
Chakula kitakutumikia kadri unavokiagiza, kitakufurahisha kama utataka furaha na kitakukera kama hutokifurahia. Furahia mlo wako mara zote..
No comments:
Post a Comment