Wednesday, September 25

Cha usiku cha leo - Kahama

   Bado tupo Kahama, na leo tulikua tunapika nyama ya kukaangwa iliyolowekwa kwenye mchanganyiko mwingi mwingina wali wa nazi. .
Hapo chini picha ya nyama ikiwa katika mchanganyiko

 Baada ya kukolea viungo, nyama ilikaangwa kwenye mafuta

   Na huu ndio muonekano wa nyama baada ya kuiva

  Na ule mchanganyiko wa kumarinate nyama ulipikwa na kutengenezwa sauce ya kulia wali 

Kusindikizia nyama zile, wali wa nazi ndio ulitumika

Matunda ya aina kadha wa kadha yaliyokatwa katwa vipande na ndio yalisindikizia menu nzima na bilauri ya maji safi baridi

Kwa pamoja mlo wetu pande za Kahama ulikua hivi usiku huu
    Tujuze cha usiku huwa wala wapi na nani? pande zipi n.k
Kutoka Kahama LJM nawajuza!!

2 comments:

  1. Ningepata mke anayejua kupika chakula kitamu kama icho mbooona

    ReplyDelete
  2. Usipate shida, ukishaoa tu mnunulie mkeo smart phone, au laptop aweze kupata access ya menu time blog na huku atajifunza, nawe utafurahia menu hizo.
    Tunashukuru kwa maoni.

    ReplyDelete