Monday, August 12

Pilau la sikukuu ya Idi

   Kutoka kwenye sikukuu hii ndefu tuliyosherekea sikukuu ya Nane nane na za idi mosi na pili, kuna mialiko ya hapa na pale ambayo ilitawala. Team ya Menu Time tulipata mualiko pande za Kimara kwa bwana Edward, ambapo alitutayarishia pilau na mchuzi wa kuku wa kienyeji.


 Memba wa Menu Time anasema ushuhuda wake ni kwamba, mara alivyokula vipande vya kuku, alijua ni wa kisasa kwa jinsi alivyo mlaini na mtamu, ila alihakikishiwa kuwa wife wa bwana Edward ndio alifanya utundu jikoni mpaka ladha ikawa hivyo. 
  Shukrani na mapenzi tele kwa familia ya Edward Marecha kwa kutualika Idi mosi nyumbani kwao.
 Tuna hakika nyote mlisherekea vyema, na tuwatakie majukumu mema ya wiki mpya.

No comments:

Post a Comment