Monday, August 12

Msosi wa nyumbani

   Baada ya mialiko ya sherehe za idi mosi tuliyokula Kimara kwa Edward na mkewe, na idi pili tulikua kwenye harusi ya bwana Junior Makame wa Tongwe records na mkewe Grace, Jumapili tukaona tukae nyumbani na kujipikilisha.
   Kwa haraka haraka mchana tuliamua kupika viazi vya kuponda, nyama ya kukaanga pamoja na mbogamboga.
   Hivi vipande vya nyama kwanza vililowekwa kwenye mchanganyiko wa ndimu, pilipili, chumvi, soya sauce, asali, kwa muda kama wa nusu saa, kisha vikakaangwa kwenye kikaangio na mafuta kidogo. Kumbuka mkato wake ni mwembamba na unarahisisha kuiva kwa pishi la aina hiyo.
  Pata picha wakati vinalowekwa
   
 Hizi mbogamboga baada ya kuchemshwa kidogo ziliungwa kwa vitunguu, nyanya pamoja na viungo na badala ya tui la nazi viliwekwa maziwa, na rojo likatokea hivyo. 
Kwa picha ya msosi mzima, sahani ilionekana hivi

     Kesho tutarejea kukujuza ni chakula kipi tulipika Jumapili jioni. Waweza share nasi nini ulipata kipindi cha sikukuu hizi, iwe ulialikwa au ulipika.

No comments:

Post a Comment