Wednesday, August 14

Menu ya nyumbani

  Tunaendelea kuwajuza mapishi tuliyopika Jumapili iliyopita tukiwa nyumbani, Kupika nako kuna raha yake ati.
  Jioni tulipika makaroni na kamba a.k.a prawns na jibini nyingi ya kutosha. 
Hawa kamba waliungwa kama mboga pembeni ila kama vile siku nzima tulipende kutumia maziwa badala ya tui la nazi, hivyo mwishoni pale ambapo inatakikana kuweka tui, sie tuliweka maziwa, tukaacha mpaka yachemke na mboga huku tunakoroga na rojo lilipoiva, tukachanganya na macaroni yaliyochemshwa pembeni na kuongeza jibini kisha tukapakua.
   Hii ni picha baada ya kuweka msosi wote kwenye hot pot halafu tukaweka extra cheese on top

   Msosi mzima unatumia takribani dk 45 hivi, ila hakikisha kwamba kamba a.k.a prawns wako wamekoshwa vyema na wamechemshwa kidogo kabla ya kuungwa. Ni hayo tu kutoka kwetu wikiendi iliyopita.
  Leo ni Jumatano ambapo tunaenda ukigoni mwa wiki, tuone kesho tunaanzaje weekend.

No comments:

Post a Comment