Sasa tumalizie yalojiri pale ambapo Airtel walifuturisha wafanyakazi wake mikoa mbalimbali, ila sisi twaripoti kutoka hapa hapa Dar iliyo salama. Karibu tumalizie...
Kwanza zilikuwepo tambi za usukari
Halafu kulikua na hili rojo, hatukudadisi sana lina nini ndani yake, maana muda haukuruhusu, tulikua busy kufuturu... upo?
Kulikua na viazi ulaya vilivyopikwa na mchuzi, kwa rangi waonekana mtamu kwa ladha ni zaidi ya utamu
Njugu mawe zenye sukari nazo zilikuwepo, zilizoungwa vyema na tui la nazi
Mihogo ndio msimu wake haswaa, nayo ilikuwepo iliyopikwa na tui la nazi na iliki kama ilivyo ada
Halafu pale ambapo wengi hupapenda kwenye ndizi mzuzu zilizopikwa kwa tui la nazi na iliki zikapikika na kukolea ladha
Uone tu mpangilio wa mezani ulivyotulia tayari kwa waalikwa kujinafasi
Kwa upande mwingine wa meza ulivyokaa, ili uone mambo mengi kwa pamoja
Kutoka Airtel house iliyopo moroco, Kinondoni, Dar iliyo salama, Tanzania hatuna la ziada zaidi ya kuwatakia siku njema na mfungo mwema wa siku chache zilizobaki za mwezi mtukufu wa Ramadhan.
No comments:
Post a Comment