Monday, August 19

Lasagna ya Iringa

   Kama ilivyoa ada yetu, kila tutembeleapo Iringa ni lazima yetu kupita na kusalimia Neema craft workshop, ili kutimiza yale maazimio tuliyojiwekea. Azmio la kwanza la kwenda pale ni kuweza kula lasagna yao ambayo bado hatujapata pahala pengine panapowashinda kwa utamu, pili kuweza kununua vitu viwili vitatu kwa ajili ya wanafamilia na tatu kuweza kuongeza chochote katika kusaidia mfuko wa Neema craft workshop.
   Hapo chini ndio Beef lasagna tuliyokula team ya Menu Time wakiwepo Lulu na Beda

   Ukipata bahati ya kutembelea Iringa, au iwapo upo Iringa twakusihi kwenda pale kwa shopping ya mambo mbalimbali, pia kwa ajili ya milo tofautitofauti kuanzia chakula cha asubuhi, bites, chai mbalimbali, juisi na kadhalika. Kuna mengi utapata pale.
   Tutaendelea kuwajuza tuliyopishana nayo katika safari yetu ya Iringa wikiendi iliyopita

No comments:

Post a Comment