Tuesday, June 25

Vyuku na mapishi yake mbalimbali

   Kuna aina mbalimbali za upishi wa kuku, awe wa kienyeji au wa kidhungu, upishi wake ni tofauti na waweza kupikika kirahisi.
   Leo tunakuonesha aina mbalimbali za vyuku na mapishi yake na wapi tulipishana nao.

   Ya kwanza ni ya kukaanga, ambapo kuku wamekaangwa kwenye mafuta na kuchujwa kisha wapo tayai kwa kuliwa. Ilikuwa kwenye sherehe ya kumonyio ya kwanza.

Ya pili ilikua pande za Postal grounds kwenye event ya Nyama choma festival, katika banda la T.bonaz. Vyuku hawa wanachomwa na kuepuliwa tayari kwa kuliwa.

   Ya tatu tulipishana nayo pande za China great wall restaurant ambapo hawa walikaangwa pamoja na mbogamboga, wakiwa served na aina nyingine ya menu uipendayo. Ilikua sherehe ya kuzaliwa ya Junior a.k.a J Murder, pia sherehe yao ya kumvisha pete ya uchumba mchumba wake Grace wa Vincent.

   Ya mwisho ni hapo hapo ila kuku  huyu kama alipikwa katika mandhari ya kuchemshwa, akiwa pamoja na mbogamboga 

   Je, wewe unapenda kumla kuku anayepikwa katika mapishi yapi? na je, wapenda kumlia ukiwa home, restaurant, hoteli n.k na je ni ipi? tujuze nasi tusheee

2 comments:

  1. Aina ya kuku ninayempenda ni wa kuchemshwa akiwa na viungo mf. tangawizi, chumvi, ndimu, kitunguu saumu. Unachemsha vyote pamoja bila kuweka maji, ikikaukia nageuza geuza . Tayari kwa kuliwa.

    ReplyDelete
  2. Asanta kwa kushare nasi, tutajaribu pishi hilo na kukujuza limetokaje.

    ReplyDelete