Jana tumeyaona mapishi ya vyuku, basi leo tuangalie nyama ya ng'ombe tukiwa pale pale Great wall restaurant iliyopo Masaki. Shughuli ilikua ileile, sema nakujuza taratibu menu tulizopishana nazo pande hiyo. Wapo Oysterbay hawa...
Hii ya kwanza, kama imefanywa kwa mapishi ya kustimu zaidi, ila vitunguu havikuachwa kukaangika sana, na pembeni kuna mboga mboga zilizochemshwa tu na kupakuliwa tayari kwa kuliwa.
Halafu kuna hii iitwayo chicken sizzler ambapo nyama hii huja ikiwa kwenye chombo cha moto kutoka jikoni kikiwa kinapiga ukelele kama vile bado vyakaangika. Chini ya sahani ya bati, kunakuwa na ubao ambapo husaidia kutoharibu vitambaa vya mezani pamoja na meza yenyewe.
Bado nafurahia upishi wao maana hawa huwa wanatumia mbogamboga zaidi kwenye mapishi yao, na wakati mlaji wavitafuna vyaonekana kama vina ubichi flani ila kwa utamu.
Tujuze wapenda kula nyama ya ng'ombe ikiwa imepikwa vipi halafu wapi unaila?
No comments:
Post a Comment