Karibuni tuanze somo:
- Changanya nyama ya kusaga ya ng'ombe na nguruwe pamoja na viungo. Hakikisha mchanganyiko umechanganyika vyema
- Baada ya kuchanganya vyema, nyama yako itaonekana hivi
- Tayarisha mikate yako, kuna watakaopenda kutumia mikate ya kawaida na wengine skonzi a.k.a loaf and buns
- Tengeneza viduara vidogo vidogo vya nyama kwa umbo la mviringo, na hapo vinakua tayari aidha kuokwa au kukaangwa
- Tayarisha mikate yako kwa kuondosha ukingo mgumu wa mikate. Weka tayari pamoja na nyama yako ambayo inapaswa kupikwa
- Katakata vipande vya nanasi, kabechi, changanya na mayonnaise, olive oil na vinegar, na muonekano wake utakua hivi
- Weka kikaangio chenye mafuta kiasi kwenye jiko na pale kinapokua na moto wa kutosha, weka nyama juu ya kikaango na ikaange kwa muda, kisha geuza upande wa pili nao uive vyema. kumbuka kutoipika kwa muda mrefu kwani yapaswa kuacha iwe na utamu utokanao na mchuzi uliomo kwenye nyama
- Chukua vipande vya mkate tayari kwa kutengeneza burger/ sandwich yako. Upande mmoja weka mchanganyiko wa mboga kama hapo juu na itaonekana hivi
- Upande wa pili weka kipande cha nyama
- Iwapo hutapenda kuweka vikorombwezo basi utakua umefika mwisho wa safari yako
- Iwapo utapenda kuongezea vikorombwezo, kina tomato, mustard na mengineyo basi itakua hivi
Na hapo utakua umefikia mwisho wa matengenezo ya sandwich/ burger ya nyama ya ng'ombe changanya na nguruwe.
Mlo huu hulika na aina yeyote ya kinywaji, kuanzia chai, juice, maziwa n.k vile utakavyoamua wewe.
Menu Time inamshukuru George kwa kushare na kutufunza mapishi haya.
No comments:
Post a Comment