Saturday, January 5

Mapishi ya Anita - Mwaka mpya

  Anita ameshare nasi kile alichopikia familia yake siku ya tarehe 1, mwezi wa kwanza katika kusherehekea mwaka mpya.
   Anasema kwa kujipanga vyema haikumchukua muda mwingi jikoni kukamilisha mapishi yote tayari kwa familia yake kupata chakula cha mchana.
   Kwenye sahani kuna wali wa njano, macaroni yenye jibini na nyama kwa mbali, kuna baked potatoes, nyama ya nguruwe iliyobanikwa, kipande cha kuku aliyekaangwa pamoja na kachumbari
  Tunaamini vyote vilienda salama katika kusherehekea mwaka mpya kwa Anita pamoja na familia yake. Tunamshukuru kwa kushare nasi mapishi na mlo walioupata.
  Iwapo ungependa kutujuza yaliyojiri sikukuu zilizopita karibu sana kupitia anwani zetu info@menutimetz.com na menutimes@gmail.com 

No comments:

Post a Comment