Tuangalie leo namna ya kubadilisha style ya mlo wa asubuhi a.k.a breakfast, ni kwamba viungo au niseme vyakula ni vilevile ila mapishi ni tofauti kidogo. Tunaongelea mapishi ya mikate iliyowekwa kwenye mayai.
Mahitaji;
- Mayai
- Maziwa kiasi
- Chumvi kiasi
- Mkate
- Blue band iwapo utapenda
- Koroga mayai, ongeza chumvi kiasi na maziwa kiasi, kisha yaweke pembeni
- Chukua kikaango weka jikoni na pasha moto jiko . Ongeza mafuta kiasi cha kijiko kimoja cha chai
- Chukua kipande cha mkate, mwagia/ lowanisha kwa juu na mayai kama inavyoonekana kwenye picha
- Ukishamaliza upande mmoja, rudia upande wa pili ambao nao unaulowanisha pia.
- Weka mkate uliowekewa mayai kwenye kikaango ambacho kimepata moto. Acha kwa dakika kadhaa ili mayai yapate kuiva vyema
- Geuza mikate upande wa pili ili uweze kuiva nao, na uache kwa dakika kadhaa kama ulivyofanya kwa upande wa kwanza. Upande wa kwanza utaonekana hivi
- Epua mikate yako tayari kwa kuliwa. Sasa waweza amua kuweka blueband au jam au chochote katika kuongezea utamu mikate yako iliyochovywa kwenye mayai na kukaangwa.
Mikate hii ni rahisi kutengeneza na hupendwa sana na watoto. Iwapo watakua wamechoka kula mlo uleule wa mikate ya blueband na yai la kuchemsha au kukaanga, basi jaribisha mpiko huu na wataendelea kula vyema.
Iwapo una namna tofauti ya upikaji wa mlo wa asubuhi haswa kwa watoto, karibu kutujuza nasi tuwajuze marafiq kokote walipo.
No comments:
Post a Comment