Friday, November 9

Serena Hotel - Food testing

  Unapokua na shughuli, iwe ni kipaimara au harusi, au shughuli ya ofisi au ya kuwajuza ndugu, jamaa na marafiki kwamba mmechumbiana, au chagua shughuli yeyote lazima uipange vyema na ipangike.
  Menu Time Investment tuna andaa shughuli mbalimbali kutokana na matakwa ya wateja wetu. Kuna kipindi tunashirikiana na wengine au pengine hufanya wenyewe.
  Leo tumehusishwa kwa namna kidogo katika shughuli ya Kampuni ya Sigara ambapo wanawatambua nyota wao yaani wafanyakazi bora wa kampuni yao.
  Jana tulihusishwa katika kipengele kimoja cha kujaribisha chakula ambacho kitaliwa siku ya leo ya sherehe yenyewe, na kifuatacho ndicho chakula tulichojaribisha. Karibu!!
   Kulikua na supu ya choroko na vikorombwezo kadhaa
 
Kisha kulikuwa na supu ya samaki
 
Halafu msosi kamili ndo ulikua hiviiii,
 
Na sahani ya Dada Jane ilikua hiviiiii, 

  Tulimaliza kuhakikisha ladha, muonekano na tukakubali kwamba menyu ya hapa ina standard ya juu. Desert hatukupiga picha ila tutakuja kuwajuza soon soon.
  Kutoka pande za Serena Hotel, iliyopo mjini dar iliyo Salama, mie ni LJM wa MT naarifu.

No comments:

Post a Comment