Monday, November 12

Pilau kutoka Kilimanjaro

   Pilau ni mlo maarufu sana Tanzania na nje ya Tanzania. Kuna aina moja ya pilau inayojulikana na wengi, na hii ni ile ya kupikia nyama pamoja na mchele au niseme wali, kisha vyote vyaiviana humohumo pamoja. Sasa kwenye upande wa nyama inategemea unaamua kupika nyama gani, kuna wanaopika na kuku, nyama ya ng'ombe, wengine ya bata na hata kuku, inategemea na mapenzi yako mwenyewe.
   Inayojulikana sana ni ile ya nyama ya ng'ombe ambapo siku za nyuma tuliwajuza namna ya kuipika. Mara nyingi pilau haikosekani kwenye sherehe.
   Katika upishi bado tunaenda tukitofautiana, kuna wanaoweka njegere na karoti ,wengine huweka tui la nazi, hizi zote ni nakshi mbalimbali ambazo zinaongeza ladha.
   Kisha kuna pilau chukuchuku, naliita chukuchuku kwasababu hupikwa pasi nyama ya aina yeyote. hapa mchuzi wa nyama huungwa pembeni, na iwapo utataka pilau ya ng'ombe unachotewa pilau chukuchuku kisha mchuzi wa nyama ya ng'ombe unaongezewa kwa juu na vipande kadhaa na unapata pilau yako. Upishi huu upo kwenye migahawa mingi sana.
  Kutoka Kilimanjaro, Moshi, Arafa wa MT alikutana na pilau za aina hii, na huu hapa ni ushuhuda wake
 
   Pembeni kuna kachumburi kama ilivyo ada, kisha kukaongezewa na mboga za majani, na hii ilikua ni pilau ya kuku, au tuseme pilau chukuchuku na nyama ya kuku... vyovyote upendavyo ni sawa.
   Karibu kutujuza wapenda pilau ya aina gani? unaipata wapi? na kama ungependa kuonesha na picha pia, tutafurahi zaidi. Anwani yetu ni info@menutimetz.com 

No comments:

Post a Comment