Bado tunaongelea wikiendi ndefu ambapo tulikua na mapumziko, Rafiqs sijui nyie mlitumiaje siku hiyo na familia zenu.
Niendeleze historia yangu mie na wanafamilia yangu tulipopata kutembelea mgahawa wa Cape town Fish market pande za msasani mjini Dar es salaam.
Mmoja wa wanafamilia alipata kuonja menu hii hapa chini, ambapo kuna viepe, kamba pamoja na ngisi, huku vyote vikisindikizwa na salad, pilipili, mayonnaise sauce pamoja na kipande cha ndimu
Na mwingine yeye alipata kula salad pamoja na kamba waliopikjwa kwenye sauce yenye uyoga, huku naye akisindikizwa na salad pembeni pamoja na kipande cha ndimu
Imeonelewa kuwa ni sahihi pale mlaji anapochagua chakula cha majini a.k.a sea food basi husindikizwa na kipande cha ndimu kwani husaidia kwenye ladha lakini pia mwishoni baada ya kula ni kiungo kizuri kinachokata shombo, au tuseme harufu ya chakula cha majini.
Kama ulikua hujui basi chukua hiyo, kwamba iwapo wataka kukata shombo yoyote mikononi mwako baada ya kupika au kula, fanya kujikamulia ndimu kidogo mikononi kisha nawa na sabuni na ile harufu itakwenda.
Tutaja wajuza tumepishana na menu gani ingine katika hii hii long weekend
No comments:
Post a Comment