Tuesday, July 8

Mambo ya wikiendi ndefu


   Tulikua na wikiendi ndefu sana iliomaliziwa na sikukuu ya sabasaba, ambapo tumepata nafasi ya kupumzika na kuweza kujumuika na wanafamilia, rafiqs na majirani na kufurahia sikukuu ya wakulima.
   Nikiwa na familia tuliamua kwenda Cape town fish market iliyopo Msasani, kwa ajili ya chakula cha usiku, na hapo chini ni baadhi ya menu zilizochaguliwa na kuliwa siku hiyo.
  Cha kwanza kilikua ni viepe a.k.a chips, salad kidogo pamoja na kamba a.k.a prawns.


 
 Pia hiki kilikuwepo ..... naongelea wali mweupe, kasalad kidogo pamoja na nyama ya ng'ombe ilopikwa vyema a.k.a well done.
   Tutaendelea kukujuza yalojiri kutoka mgahawa huo hapo kesho.

No comments:

Post a Comment