Wednesday, March 12

Ugali mweupe

   Leo twaangallia ugali, mlo wetu wa kitanzania kabisa, wa kinyumbani upendwao na wengi na pia huliwa na wengi huku tukitofautiana kwenye mboga.
   Leo tumekula ugali wa mahindi, dagaa walioungwa kwa nazi na kupikwa na nyanya chungu 
pamoja na mlenda, huku tukishushia na maji safi ya kunywa

       Tujuze wapenda kula ugali na mboda gani? je, wapika mwenyewe au waenda sehemu kula tujuze ni wapi nasi tujumuike.
     Twawatakia Jumatano njema yenye baraka tele.

2 comments:

  1. Napenda kula ugali samaki wa tui la nazi na maharage yaliyoungwa na mafuta na kitungu, karoti, hoho na mchicha wa mafuta na kitunguu tu

    ReplyDelete