Thursday, March 13

Ugali dona

  Hivi imewahi kukutokea kwamba kuna menu flani hujawahi kuila toka umezaliwa ilihali inapatikana unapoishi? Aidha inakua wazazi wako hawakukulisha au ni kwamba ulikua hukutani navyo, pengine hukuvipenda au wazazi hawakuvipenda au hawakuvitilia maanani, maana tuwapo wadogo, maamzi ya leo kipikwe nini yapo mikononi mwa wazazi mpaka pale nasi tunapokuwa na kwetu na maamuzi yetu ya leo tunakula, hatuli na kama twala basi twala nini yanakuwa ni juu yetu ni si wazazi wetu tena!
  Mmoja wa wana Menu Time hakuwahi kula mlenda hadi hivi juzi alipopishana nao sehemu na kuanza kuugida kwa pupa.
  Maelezo yake ni kwamba una ladha ya ajabu yani ya pekee na alipoujaribu, aliula kwa siku nne mfululizo bila kuuchoka huku akisindikiza na ugali,  samaki alioungwa na tui la nazi na mboga mboga nyinginezo.
  Hapa chini ni ushuda wa moja ya milo yake alipofumania mboga ya mlenda na kuipenda


  Ugali ni ule wa dona, na mboga mboga zilizosindikiza mlenda ni spinach pamoja na keabichi

   Tujuze ni menu ipi umeanza kuila ukubwani kupitia menutimes@gmail.com, pia tufwate instagram kupitia @menutimes kupata kujua yalojiri hapo kwa hapo na team ya Menu Time.
  Twawatakia Alhamisi njema!!

No comments:

Post a Comment