Tuesday, March 11

Asubuhi hii tumefungua menu hivi

    Leo asubuhi tumejipikilisha kabla ya kukutana na majukumu ya siku hii. Ni chakula rahisi kupika na takribani yachukua nusu saa toka kutayarisha, kupika hadi kupakia kwa ajili ya kufungua kinywa tufanyiapo kazi.
   Tumepika mayai ya kuvuruga a.k.a scramble eggs ambayo yana vitunguu maji, nyanya, pilipili hoho, jibini, mayai, chumvi kidogo pamoja na mafuta ya kupikia.
   Kisha tulipika chapati maji a.k.a pancakes ambapo siku za awali tulionesha matayarisho na namna ya kupika. Hizi za leo zina mayai, maziwa, unga wa ngano, asali kidogo, chumvi kiasi na kukaangwa na mafuta ya kupikia.

   Hapa ni baada  ya kupakia vyema tayari kwa safari, tulipofika sasa kabla ya kupakua mlo ulionekana hivi, ukiwa tayari kushushiwa na chai ya maziwa

       Na hapa ni baada ya kupakua menu ikiwa tayari kwa mlo wa asubuhi.
 
   Tujuze ni menu gani Rafiq hujitayarishia kabla ya kuanza majukumu yako ya kila siku ya kujenga taifa. Tutumie kupitia menutimes@gmail.com

No comments:

Post a Comment