Tuna wagonjwa basi tupo kimya tunalea. Ila leo tumewamiss mno na tukaona tushare nanyi kifungua kinywa cha leo.
Showing posts with label Menu Kitaani/Nymbani. Show all posts

Thursday, July 3
Wednesday, July 2
Mtori wa mgonjwa
Tukiwa tunalea wagonjwa tumeletewa mtori na mama wa mama Menutime, yaani bibi Menutime. Mtori ni moja ya chakula ambayo ni rahisi kupika na pia kuliwa na mgonjwa maana anafanya kumeza tu ambapo hahitaji kutafuna sana.
Basi leo tumeletewa mtori na bibi na huu ni kama ule wa nyumbani Rombo, maana sie si wachagga ivo tukarejea nyumbani.

Kwenye makala zetu huko nyuma tumewajuza namna ya kupika mtori, karibu ujifunze usipate shida kumlea mgonjwa wako nyumbani au hata hospitalini iwapo utapaswa kupeleka menu.
Twawapenda sana sana, na twamtakia mgonjwa wetu apone haraka.

Thursday, June 26
Menu ya kinyumbani
Bado twapokea picha toka kwa Rafiqs, na kushare nanyi, na pia mapishi bado yako kutoka majumbani mwa watu, yaani hatupo kitaani.
Kutoka kwa Rafiq ambaye hakutaka kujulikana ameshare nasi menu toka nyumbani.
Hapo juu kuna wali, maharagwe, mboga za majani na kachumbari. Pembeni kuna kikorombwezo cha pilipili.
Karibuni kushare nasi.

Wednesday, June 25
Ndizi nyama
Baada ya kutoka Kigambonino,bwana Abdallah wa Gunda ameshare nasi menu ya nyumbani ambapo alipikiwa na dada mmoja wa kichagga.
Ilikua ni ndizi nyama na picha ya kwanza zikiwemo bado ndani ya hotpot
Halafu hii ya pili ikiwa ndani ya sahani tayari kwa kuliwa.
Karibu kushare nasi menu unazozipata popote pale, kupitia menutimes@gmail.com hata watsup kwa namba hii 0784 999 790.

Monday, June 16
Mambo ya Wikiendi
Kuna mengi hufanyika mwisho wa wiki a.k.a wikiendi, na katika yote hayo la muhimu ni kusali, kula na kulala katika muda ujipangiao wewe mwenyewe pasi kushurutishwa na mwanaadamu yeyote.
Katika wikiendi hii tulipata tembelea maeneo mbalimbali na tutashare nanyi menu zote tulizozipata pale tulipoketi na kuonja utamu waoutengenezao wapishi wa menu hizo.
Kutoka Nyumani Lounge, mgahawa uliopo karibu na Best bite tulipata menu hii hapa, kuna ndizi na mishkaki. Mishkaki hii ni firigisi,, huku ikisindikizwa na kachumbari na pilipili.
Pia wanatuarifu kuwa siku hizi kuna soseji zile kubwa kubwa, katika upishi uuchaguao wewe mwenyewe na mapenzi yako. Sisi tuliagiza za kukaanga pamoja na vipande vya kuku, na mtazamo wa sahani yetu ndio ulikua hivyo hapo chini. Kama ilivyo ada, shurti kachumbari na pilipili visindikize menu nzima.
Tulipata kutembelea sehemu kadha wa kadha na zote tutashare nanyi, kwasababu tunawajali na kuwapenda na tungependa nanyi mkaonje hayo tuliyoyapata.
Tukutane kesho!!

Monday, June 2
Monday, May 5
Mchemsho wa kinyumbani
Tuanze wiki vizuri huku tukiujenga mwili vyema baada ya mapumziko ya siku hizi mbili. Tunatofautiana na namna tupumzikavyo, ila mwisho wa siku Jumatatu ndiyo hii na shughuli zinaendelea kama kawaida.
Leo waweza anza siku namna hii, au hata ukaweza kuipata kama menu ya mchana.
NI rahisi maana humu kuna kuku wa kienyeji, viazi vya kuchemsha, karoti, brokoli pamoja na mboga nyinginezo ambazo mwenyewe utapenda kuongezea.
Kisha wachemsha tayari kwa kuandaa kama mlo
Wale wasiopenda vyakula vyemye mafuta, au vya kukaangwa, huu ni mlo mzuri sana kwao, pia kwa wale wanaotengeneza miili yao isinenepe bila sababu.
Tunawatakia wiki njema yenye mafanikio kwenu

Thursday, May 1
Nyumbani ni Nyumbani
Bado tuko Nyumbani Lounge tunaangalia menu nyingine ipatikanayo pale
Kuna pancakes a.k.a chapati maji na rosti ya firigisi
Mchana wanakuwaga na chakula cha mchana katika mtindo wa buffet. Wasalimie ukiwa pande zile au fanya sababu ya kuwepo pande zile.
Twawatakia Sikukuu njema ya Mei Mosi
Wednesday, April 30
Kutoka Nyumbani Lounge
Kutoka mgahawa wa da Jaydee, mlo tuliopishana nao jana ni huu hapa..... kuna ugali, firigisi rosti pamoja na sukumawiki
Fanya kupita hapo leo
Fanya kupita hapo leo
Tuesday, April 29
Menu ya kinyumbani
Leo tupo na menu ya nyumbani ambapo tuna wali wa samaki, maharagwe, tudagaa kwa mbali na ndizi kama tunda.
Karibu tule chakula cha nyumbani.
Karibu tule chakula cha nyumbani.
Saturday, April 5
Nyumbani lounge
Moja ya menu utakua umepishana nayo Nyumbani lounge ni mchemsho wa kuku wa kienyeji, ulipikwa na ndizi na viungo vingine mbalimbali.
Kwa ushahidi wa karibu utapata mchemsho uonekanavyo hivi hapo chini

Tuendelee kukutana Nyumbani lounge, kupata menu mbalimbali tamu za kiafrika na muziki muzuri.
Tunaelekea Arusha na Moshi tufwate kwenye instagram kupitia @menutimes na twitter ni @menutimetz kupata latest updates.
Twawatakia wikiendi njema.

Monday, March 31
Menu ya nyumbani
Kutoka nyumbani kwa mama Lulu, mwisho wa wikiendi huu tulipata moja ya menu alizotutayarishia. Hii ni viazi kaanga na samaki kaanga, huku wakisindikizwa na kajikachumbari hivi.
Wiki yako iliishaje Rafiq??? Tujuze kupitia menutimes@gmail.com
Posted via Blogaway
Monday, March 24
Kifungua kinywa
Tumeamkaje asubuhi hii? Naamini tupo salama kabisa.
Karibuni supu

Karibuni supu
Vikiwa kwa pamoja

Ni supu ya kuku yenye vikorombwezo
Inapatikana Nyumbani lounge.
Inapatikana Nyumbani lounge.
Tunawatakia Jumatatu njema na wiki njema.
Thursday, March 20
Wednesday, March 19
Wali kuku
Jana usiku tulijipikilisha nyama ya kuku iliyosagwa, ambapo ilipikwa kama mboga ya kawaida na kumaliziwa na tui la nazi, huku ikisindikizwa na wali wa nazi.
Pembeni kulikua na maji safi ya kunywa.
Karibuni nyumbani kwetu.
Pembeni kulikua na maji safi ya kunywa.
Karibuni nyumbani kwetu.
Tuesday, March 18
Yalojiri wikiendi iliyopita
Tunaendelea kukujuza wikiendi yetu. Hivyo basi cha usiku tulikipata pande za Nyumbani Lounge tukiwa na marafiqs
Tunawatakia Jumanne yenya Amani
Tunawatakia Jumanne yenya Amani
Monday, March 17
Menu za nyumbani wikiendi iliyoisha
Tunaamini wikiendi ilimalizika vyema na salama kwetu sote. Na twaanza wiki tukiwa na nguvu mpya.
Moja ya menu tulipata kuzila wikiendi iliyopita ndio hizo hapo chini.
Tulifungua kinywa namna hii, kwa chapati maji zenye syrup ya ladha ya chokoleti, kitumbua kimoja, kipande cha jibini na chai ya maziwa.
Mchana tulipata kula menu tuipendayo siku za Jumamosi pande za Shieni bar. Na menu hiyo ni kuku rosti asopikwa na mafuta, alochanganywa mchicha, pamoja na ugali wa dona.
Pata muonekano wa picha hapo chini
Tujuze wikiendi yako ulikula nini? na uliipatia wapi?
Kesho tutakujuza usiku tulipata nini.

Tuesday, March 11
Asubuhi hii tumefungua menu hivi
Leo asubuhi tumejipikilisha kabla ya kukutana na majukumu ya siku hii. Ni chakula rahisi kupika na takribani yachukua nusu saa toka kutayarisha, kupika hadi kupakia kwa ajili ya kufungua kinywa tufanyiapo kazi.
Tumepika mayai ya kuvuruga a.k.a scramble eggs ambayo yana vitunguu maji, nyanya, pilipili hoho, jibini, mayai, chumvi kidogo pamoja na mafuta ya kupikia.
Kisha tulipika chapati maji a.k.a pancakes ambapo siku za awali tulionesha matayarisho na namna ya kupika. Hizi za leo zina mayai, maziwa, unga wa ngano, asali kidogo, chumvi kiasi na kukaangwa na mafuta ya kupikia.
Hapa ni baada ya kupakia vyema tayari kwa safari, tulipofika sasa kabla ya kupakua mlo ulionekana hivi, ukiwa tayari kushushiwa na chai ya maziwa
Na hapa ni baada ya kupakua menu ikiwa tayari kwa mlo wa asubuhi.
Tujuze ni menu gani Rafiq hujitayarishia kabla ya kuanza majukumu yako ya kila siku ya kujenga taifa. Tutumie kupitia menutimes@gmail.com

Monday, March 10
Kutoka Nyumbani Lounge
Ni Jumatatu nyingine tulivu, ambapo tunaanza wiki taratiibu tukiwa na mengi tuliyoazimia kuyatimiza.
Mwisho wa wiki iliyopita tulipita Nyumbani Lounge, ule mgahawa wa Rafiq zetu na menu tuliyopishana nayo ni pamoja na
Samaki spesho kama aonekanavyo hapo chini
Tunawatakia kila la kheri kuyatimiza yote myatarajiayo.
Mwisho wa wiki iliyopita tulipita Nyumbani Lounge, ule mgahawa wa Rafiq zetu na menu tuliyopishana nayo ni pamoja na
Samaki spesho kama aonekanavyo hapo chini
Tuesday, March 4
Chakula cha mchana toka Nyumbani Lounge
Jana tulipata mlo wa mchana mgahawa wa Nyumbani Lounge, na pale huwa panakuwa na buffet, yaani milo tofauti ambapo wapakua tani yako, na menu uipendayo.
Sahani yetu ilikua hivi
Kuna wali mweupe wa nazi, kuku kaangwa, rosti ya ng'ombe, mchicha uliokaangwa na vitunguu maji na karoti, pamoja na ugali wa muhogo.
Vyote vilishushiwa na maji ya matunda baridi, na mchana ukapita vyema.
Karibuni Nyumbani Lounge kwa mlo wa mchana, wa usiku, snacks, bites, vinywaji mbalimbali, na burudani nzuri ya bendi ya Machozi band siku ya Ijumaa, na muziki mchanganyiko kila usiku.

Subscribe to:
Comments (Atom)