Monday, January 20

Cha usiku kutoka kwa Mama Lulu

Usiku wa leo tumepata kula wali wa nazi, nyama ya kusaga iliyoungwa na maziwa, mchicha ulochemshwa pamoja na mtori pembeni.

Sasa basi kwa sababu mimi ni kitinda mimba a.k.a mtoto wa mwisho, huwa nahesabiwa katika chakula cha watoto wa ndugu zangu, kikipikwa wanapokuja msalimia bibi, na ndio sababu ya kuwa na kamtori kidogo.
Kisha tukamalizia na desert ambapo ni vipande vya maembe yaliyochangnya na  mtindi wenye ladha a.k.a yoghurt. 



Twawatakia usiku mwema Rafiqs.

No comments:

Post a Comment