Kutoka wanafamilia wa Menu Time hivi ndivyo tulivyosherehekea sikukuu ya Noeli.
Kulikua na kuku waliochomwa na muka ya Ringo, a.k.a mama Anya baada ya kulowekwa kwa viungo
Pia aliwakilisha vyuku katika staili ingine ambapo hawa waliookwa kwenye oven baada ya kuloweshwa kwenye viungo
Da Salma, naye alitutengenezea meat balls, humo kuna mashed potatoes, nyama iliyosagwa na mbwembwe nyingine
Mbuzi choma, iliyochomwa kule Shieni bar iliyopo Sinza nayo ilikuwepo
Nguruwe iliyotengenezwa katika mtindo wa rosti na bwana Ringo a.k.a baba Alexia ilikuwepo
Nguruwe iliyookwa ndani ya oven na muke ya Ringo nayo ilikuwepo na ilikua tamu munoo
Mama Menu time alihakikisha uwepo wa prawns salad yenye viazi, karoti pamoja na njegere, huku vyote vikachanganywa na mayonnaise
Pilau ya ng'ombe kutoka mkono wa mama Seif, a.k.a mamaake a.k.a muke ya Papaa lilikuwepo
Salad na kachumbari havipishani sana, hivyo Mama Menu time a.k.a Mama Mangi alisimamia kachumbari ya kulia pilau. Kulikua na vitunguu maji, nyanya, chumvi na ndimu. Upo?
Chaguo lilikua ni lako, na kwa kidogo moja ya sahani zilizopakuliwa zilikua hivi.....
Tunaamini nanyi pamoja na familia zenu mlipata mlo mzuri, na pia mlifurahia sikukuu vyema huku tukikumbuka kuwasalia wagonjwa na waliotutangulia na kuwasaidia wasio na uwezo. Na hii ndio maana halisi ya sikukuu ya Noeli, kumtukuza Mungu na kuimarisha Amani duniani.
No comments:
Post a Comment