Tuesday, December 10

Menu ya Kitaani

   Tukiwa tunakaribia mwisho wa mwaka, katika mahanjumati tunaonesha je, ni menu gani waweza pika au kupata katika mitazamo tofauti.
   Tulikuwa kimya kidogo kutokana na matatizo ya hapa na pale, ila sasa tumerejea vyema na salama na tupo pamoja.
   Ya mchana menu yetu ni wali mweupe, maharagwe kidogo, mchuzi na samaki wa kukaanga

   Kwa wasio na mapenzi ya samaki siku ya leo, basi kuna pilau, ikisindikizwa na mchuzi, maharagwe kidogo pamoja na nyama ya kukaanga

   Pata na soda, maji safi ya kunywa, maji ya matunda au kishushio chochote ukipendacho.
Kesho tutaja kuwajuza namna ya kupika viazi pondwa pamoja na mboga yake ilopikwa pande za Bulyanhulu tulipokwenda salimia mwisho wa wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment