Jana tulialikwa kwenye maulid ya harusi ya mdogo wetu Munira ambaye aliolewa siku ya ijumaa iliyopita. Basi tukajumuika na ndugu zetu wengi katika kukamilisha shughuli ile, shukrani sana kwa Anko Lilah na mkewe Anti Rukia kwa mualiko huu.
Shughuli ilifanyika pande za Mnazi mmoja ambapo ilianza swala na kisha ikaja menu, bi harusi aliingia na wazazi wakazawadiwa kwa kukuza binti, pia binti alizawadiwa na tukacheza muziki kidogo kabla ya shughuli kufika ukingoni.
Kila kitu kilipendeza, sio ukumbi, waalikwa, chakula, bi harusi ndo alitia fora, alipendeza muno.
kwenye upande wa maakuli, yalojiri ndio kama kwenye sahani hapo chini inavyojieleza
Yaliyokuwemo biriani, ndizi mzuzu tamuu (ugonjwa wa Ljm), ndizi mshale zilizopikwa na utumbo (zilikua tamu mno, nyama ilikua laini kupindukia) pamoja na vikorombwezo vya pilipili kali pamoja na achali ya maembe.
Tulishushia na maji au soda, upendavyo wewe na shughuli ikaishia hapo.
Karibu kushare nasi msosi unaoupata katika shughuli mbalimbali za harusi, kipaimara, maulidi, sherehe ya kuzaliwa, kuhitimu masomo nk, kupitia anwani yetu menutimes@gmail.com
Twawatakia wiki njema yenye mafanikio!!
No comments:
Post a Comment