Tuesday, November 19

Sherehe ya Simon na Bertha

Jumamosi tulikua na kasherehe kadogo pande za kwa mama Lulu, na kama ilivyo ada Menu Time iliitwa kusimamia mambo ya menu. 
Tukafika on time, tukapika, tukatayarisha,ili kuwapa raha wanafamilia waliofika kujiunga na sherehe ya wenetu ya kufikisha mwaka mmoja.
  Tunawaongelea mapacha wa nje, yaani bwana Simon na Bi Bertha, wao walizaliwa tarehe 14 ya mwezi wa 11 mwaka 2012, hapa hapa Dar iliyo salama. Team Menu Time inawatakia kila la kheri katika maisha yao na pongezi nyingi kwa wazazi kwa kukuza vyema.
   Yalojiri mezani ni kama ionekanavyo kwenye picha ya pamoja kisha chini tunachambua chungu kimoja baada ya kingine 

    Kulikua na pilau ya kuku, iliyokolea viungo huku rangi ikibaki ya kawaida kidogo. 

  Kachumbari ya kusindikizia pilau ambayo ilinogeshwa na mayonnaise

  Kulikua na fish balls, ambazo kama ilivyo ada ya wanafamilia, huwa hamnaga kiporo chake

  Kulikua na vyuku vilivyolowekwa kwenye mchanganyiko wa viungo na kisha kukaangwa tayari kwa mlo

Sasa katika sahani ya Mama Menu Time mwenyewe mpango mzima ulikua kama ionekanavyo hapo chini. Mtindo ni kupakua kiduchu kiduchu kila section huku wajisindikiza na tunda


  Kama una sherehe ya wanafamilia, marafiki ambapo hutaki kujichosha kupika, basi karibu kututafuta ukitupatia menu utakayo tukupikie nasi tutahakikisha shughuli yako ipo sawa. Anwani yetu ni menutimes@gmail.com au tupigie +255 784 999 790 tusemezane.
 Tutakuja kesho kuwaonesha je ni keki zipi tuliwatayarishia???? Jiunge asi kesho.

No comments:

Post a Comment