Wednesday, November 20

Keki za birthday ya Simon na Bertha na ........

  Baada ya kuona ni menu gani tulifurahia ile siku ya Jumamosi ambapo tulikuwa twashekea siku ya kuzaliwa kwa wenetu Simon na Bertha a.k.a mapacha wa nje, ukaja ule wasaa wa kukata keki, ambapo chokolate cake iliandaliwa kwa ajili yao.
  Hapo chini kuna hizo keki mbili ambapo ya Simoni ilikua na pambo la Spider man huku ya bi Bertha ikiwa na pambo la Barbie girl.

   Tuitathmini kwa karibu zaidi keki ya bwana Simon

   Kisha tuitathmini ya bibie Bertha, ambapo kwa utamu zote zilikua sawa.

    Tukawa na kasuprise kwa mashangazi na mama wakubwa wa kina Bertha pamoja na Simon. Wote ilipotimu siku yao ya kuzaliwa hawakupatiwa keki, basi tukawaletea keki ya kiutu uzima.... yaani chini chokoleti tupu kisha juu imemaliziwa na matunda ya strawberries, zilizochovywa kwenye chokolate syrup kabla ya kupangwa hapo juu

   Inajulikana kwamba mchanganyiko wa hivi vyakula viwili yaani chokoleti na strawberries, matokea yake ni balaaaaaa, na hilo tulishuhudia siku ya Jumamosi.
  Kumradhi picha ilipigwa baada ya baadhi ya matunda kuliwa.... ilikua ngumu kuzuia walaji kujipatia utamu

  Huwezi amini kwamba mpango mzima wa hiyo keki hapo juu, yenye matunda na ya kiutu uzima gharama yake ni shilingi 35,000/= tu. 
  Tujuze kama waitaka kwa anwani yetu au tupigie simu, nasi tutahakikisha utamu wa keki ya chokoleti na matunda ya strawberries unaupata.

No comments:

Post a Comment