Tulianza hivi..
Matunda kwanza, kisha tukajipa kama dakika 15 ya kuruhusu matunda yasettle kabla ya kuendelea kufungua kinywa, matunda hayo ni pamoja na vipande vya tikiti maji, embe, ndizi na nanasi
Kisha tukaendelea na kahawa ya maziwa, pamoja na croissants na andazi, huku maji ya matunda yakingoja
Kisha tukafwata mayai yalokorogwa huku yakiwekwa viungo hivi, vitunguu maji, maziwa, jibini na mafuta kidogo
Mlidhani hakutakuwepo na kanyama kokote?? mngeshangaaje?? tulimalizia na sausage za kuku katika kukamilisha kifungua kinywa chetu
Baada ya kuona ni menu gani tulifungua nayo kinywa, tutarejea kesho kuwaonesha ni menu gani tulipata wakati wa mchana.
Shukrani kwa Divas wa Airtel tuliojumuika nao, ilikua siku nzuri na yenye mafanikio maana tulijifunza mengi na mengine tutaja wajuza.
Swali moja tujiulize, Je, tunapata mlo kamili?, katika muda sahihi?, kwa ujazo sahihi?, na kukiondosha miilini mwetu katika muda na idadi sahihi??
Tutaja kuwajuza ratiba nzima ili tuone je, tupo vizuri au kuna seheme twahitaji kujiongeza, kupunguza na kadhalika.
Wiki njema yenye Baraka na Mafanikio tunawatakia
No comments:
Post a Comment